Na, Paulina Mpiwa, Sengerema- Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya sengerema mkoani Mwanza Bwn, Emmanuel Kipole amemwagiza mkurugenzi
mtendaji wa halimashauri ya Buchosa
Wilayani Sengerema kuwasimamisha kazi walimu wawili wanaotuhumiwa kuwapatia ujauzito
wanafunzi.
Amewataja walimu hao kuwa ni mwalimu Robert Malewa Albano wa shule ya Sekondari Iligamba anayetuhumiwa kumpatia ujauzito mwanafunzi wa
kidato cha kwanza na kukatisha masomo
yake huku , na mwalimu wa shule ya
Msingi Kasisa Oscar Mkandya
akituhumiwa kumpatia ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu kisha kumshawishi
kutoa ujauzito huo.
Kauli hiyo ameitoa
katika Kata ya Nyehunge
Halimashauri ya Buchosa wakati
akizungumza na watendaji wa halimashauri pamoja na madiwani
wa halimashauri hiyo kuhusu suala la kusimamia elimu katika maeneo yao.
Kipole amesema kazi ya walimu ni kuwalea wanafunzi
katika maadili mema kuwafundisha ili wapate elimu bora na hakuna mtaala unaelekeza
mwalimu kumpatia ujauzito mwanafunzi.
Amesema viongozi wote wanapaswa kusimamia sheria kanuni na maadili ya utumishi wa Umma kwa kufanya kazi
kwa weledi mkubwa.
Upande wake Mkurugenzi wa Halimashauri ya Buchosa Bw. Crispin Luanda, ameahidi kutekeleza agizo
hilo lililotolewa na mkuu wa wilaya ili kudumisha nidhamu kwa watumishi wote wa umma.
0 Response to "TUHUMA ZA KUWAPATIA UJAUZITO WANAFUNZI SENGEREMA ZAWASIMAMISHA KAZI WALIMU WAWILI. "
Post a Comment