Na Salvatory Ntandu
KAHAMA
Halmashauri ya Mji wa Kahama
leo imewasimamisha kazi Wakuu wa idara ya Usafi na Mazingira kwa kushindwa
kutekeleza majukumu yao ya kusimamia usafi na mazingira ya mji huo.
Akizungumza na Kahamafm
Mkurugenzi wa Halmashauri ya hiyo ANDARSON MSUMBA amesema waliosimamishwa kazi
ni pamoja na Mkuu wa idara ya usafi na mazingira MARTINE MASELE, Afisa afya DEOGRATIUS
DOTTO, na afisa mazingira JOHANNES MWEBESA.
MSUMBA amesema
Watumishi hao wameshindwa kusimamia
usafi na mazingira na kupelekea mrudikano wa taka katika vizimba hali
inayoweza kuhatarisha usalama wa afya za wananchi kutokana na vizimba hivyo
kuwa karibu na makazi ya watu.
Amefafanua kuwa
katika kizimba cha Milangokumi, na kwamamafarida kuna taka nyingi zilizosambaa
ovyo ikilinganishwa na vizimba vya Nyahanga na Nyihogo na amewahakikishia
wananchi usalama kwani taka hizo zitakuwa zinazolwa kila siku.
Mbali na hilo
MSUMBA ametoa rai kwa wananchi kutunza mazingira katika maeneo yao ikiwa ni
pamoja kuwa na vipokea taka.
Uamuzi huo
umefikiwa baada ya jana Naibu Waziri wa
nchi Ofisi ya Makamo wa Raisi Mazingira LUHAGA MPINA kufanya Ziara ya kukagua
usafi wa mazungira katika Halmashauri ya
Mji hiyo.
0 Response to "UCHAFU WA MAZINGIRA KAHAMA WATUMBUA VIGOGO WAWILI WA IDARA YA USAFI"
Post a Comment