Na, Paulina Mpiwa, Geita.
Baadhi ya abiria katika
kituo cha magari madogo Mkoani Geita
wamewalalamikia tabia
ya baadhi ya madereva kuwakatia tiketi
na kushindwa kuondoka kwa wakati,
jambo ambalo linasababisha kuchelewa safari zao.
Wakizungumza na Mulika Jamii abiria
hao wamesema
pindi wanapofika katika kituo hicho madereva wa vyombo
hivyo huwaagiza wapiga debe kuwapokea
abiria kwa kuwavuta kwa nguvu kupanda usafiri wao
na kuchelewa kuondoka, kitendo ambacho wamedai kuwa ni unyanyasaji wa abiria.
Madereva wa vyombo vya
moto wamekiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema kuwa kwa sasa wamekaa kikao na kuweka utaratibu
mzuri wa kuanza safari zao mapema ili kuondoa usumbufu unaojitokeza kwa sasa.
Nae mwenyekiti wa chama
cha madereva mkoa wa Geita
Bwn, Faustine John ,amesema
kuwa suala la wapiga debe kuwanyanyasa abiria halikubaliki kwa kuwa kazi yao kubwa ni kuwaonyesha abiria
usafiri pekee na si vinginevyo.
Kwa upande wake Afisa Leseni
mkoa wa Geita Bwana, Haghai Emil amewataka
abiria pale wanapokumbana na changamoto ya kucheleweshwa safari zao
watoe taarifa katika idara husika ili watu hao wachukuliwe hatua zaidi
za kisheria.
0 Response to "ABIRIA WALIA KUCHELEWESHWA SAFARI ZAO MKOANI GEITA."
Post a Comment