Na Paulina Mpiwa, Sengerema Mwanza.
Halimashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza imetajwa kuwa ya kwanza
kati ya halmashauri saba za mkoa wa mwanza katika utoaji wa huduma
bora za afya kwa wananchi katika maeneo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bwn,
Emmanuel Kipole amesema hayo katika kata ya Nyehunge halimashauri ya Buchosa
alipokuwa kizungumuza na watendaji wa halimashauri hiyo katika kuweka mikakati
madhubuti ya kuzidi kuboresha huduma za afya.
Amesema kuwa Buchosa imetangazwa kuwa ya
kwanza katika kuboresha vituo vya afya na huduma nzuri kwa wananachi katika kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongera pamoja na katibu tawala wa
mkoa.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halimashauri hiyo Dr Ernest Chacha amesema kuwa usimamizi
, na ufuatiliaji kutoka timu ya halimashauri ikiongozwa na mganga mkuu
pamoja na kushirikiana na watumishi wa afya katika halimashauri hiyo ndiyo
umeifanya Buchosa kuibuka kidedea katika
mkoa wa mwanza.
Aidha baadhi ya wananchi wa eneo hilo
wamepongeza hatua hiyo na kuiomba wizara ya afya kuendelea kuboresha zaidi
huduma zake hasa dawa ili kumrahisishia
mwananchi wa kipato cha chini kupata huduma zote muhimu katika vituo vya
kutolea tiba vya serikali.
0 Response to "HALMASHAURI YA BUCHOSA SENGEREMA YAIBUKA KIDEDEA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA MKOA WA MWANZA."
Post a Comment