SHIDA YA MAJI NYANG'WALE YASABABISHA KIFO CHA MWANAMKE KWA KULIWA NA FISI


fisi anayedaiwa kusababisha kifo cha Mwanamke kahama 


Na salvatory kelvin
KAHAMA
Mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la MARIDADI anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 Mkazi wa Kijiji cha Nyang’wale katika Halmashauri ya Mji wa Kahama na ambaye alijeruhiwa vibaya na fisi leo alfajiri akienda kuteka maji, amefariki dunia.

Akithibitisha kifo hicho, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama, DR. EMMANUEL KADELYA ameiambia Kahama FM jioni hii kuwa MARIDADI amefariki dunia wakati akisafirishwa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.

Mapema leo mchana, Daktari wa upasuaji katika chumba cha upasuaji cha hospitali hiyo, Dr. GEORGE MASASI alisema MARIDADI alifikishwa katika hospitali hiyo majira ya saa 3 asubuhi akiwa mahututi kutokana na majeraha makubwa aliyosababishiwa na fisi huyo.

Mwandishi wetu aliyetembelea Hospitali ya Wilaya ya Kahama mapema leo asubuhi alishuhudia Mwanamke huyo akiwa hajitambui akiwa amenyofolewa pua, taya la juu kulia, jicho la kulia pamoja na baadhi ya nyama katika shavu la kulia huku ulimi wake ukining’inia nje.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "SHIDA YA MAJI NYANG'WALE YASABABISHA KIFO CHA MWANAMKE KWA KULIWA NA FISI"

Post a Comment