Na,Paulina Mpiwa ,
Sengerema Mwanza.
Imeelezwa kuwa
bei ndogo ya zao la pamba,
pembejeo mbovu na mbolea kupanda
bei ni chanzo kikubwa
kilichosababisha wakulima
wengi wa zao la pamba
Wilayani Sengerema mkoani Mwanza
kuacha kulima zao hilo.
Kauli hiyo imetolewa na
baadhi ya wakulima wa zao la pamba Wilayani Sengerema ambapo wamedai kuwa
licha ya kutumia gharama kubwa kulitunza zao hilo ,lakini huuza kwa bei ndogo hali
inayowakatisha tamaa kuendelea kulima.
Wakulima hao wameeleza
kuwa kama serikali itaongeza bei ya
pamba ,kuboresha pembejeo na kushusha
bei ya mbolea wataendelea kulima zao hilo kwa kuwa ndio mkombozi kwa wakulima kama
zao labiashara.
Hata hivyo wameiomba
serikali kutazama kilimo cha pamba kwa jicho la tatu ikiwemo kukifufua kwa kutoa mahitaji muhimu ya zao hilo mapema pindi msimu
wa kilimo cha pamba unapofika
ili wakulima waondokana na
umasikini.
Kwa upande wake Mkuu wa
wilaya ya Sengerema ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Kamati ya Pamba Wilaya Bwn,Emmanuel
Enock Kipole amekiri kuwepo kwa baadhi
ya changamoto hizo na kusema kuwa serikali tayari imekwishaliona hilo na mpaka sasa
baadhi ya changamoto zimeanza kufanyiwa kazi ikiwemo wakulima kupatiwa mbegu zenye ubora.
Aidha Bwn. Kipole amesema suala la bei serikali
pia inaendelea kulishughulikia ili kuhakikisha mkulima wa zao la pamba ananufaika
na kilimo hicho kwa kuuza kwa bei inayokubalika
0 Response to "BEI NDOGO NA PEMBEJEO MBOVU ZAWALIZA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA SENGEREMA."
Post a Comment