ALIYEJARIBU KUBAKA MTOTO WA MIAKA 8 AHUKUMIWA JELA MIAKA 20




KAHAMA
Na Salvatory Kelvin
 Mkazi wa Kitongoji cha  Buyange Kijiji cha Ikinda wilayani Kahama LUCAS SAMSON(40), leo amehukumiwa kwenda jela miaka 20 kwa kosa la kumdhalilisha mtoto wa kike wa miaka 8 kwa kumwagia mbegu za kiume sehemu zake za siri.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya hiyo, IMANI BATENZI baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Mashitaka pamoja na Ripoti ya uchunguzi wa Daktari. 

BATENZI amesema Mahakama imetoa adhabu hiyo licha ya SAMSON kushindwa kuongea na kwamba mahakama haiwezi kusita kutoa adhabu kwa mtuhumiwa kwa sababu ushahidi uliotolewa unatosheleza kumtia hatiani.

Awali Mwendesha Mashitaka wa Polisi, SAADA ADAM amesema katika shauri hilo nambari 780/2016 kuwa SAMSON alimdhalilisha mtoto huyo Desemba 16 mwaka jana katika kijiji hicho cha Ikunda kwa kumwagia mbegu za kiume katika sehemu zake za siri.

Hakimu BATENZI amesema SAMSON atatumikia kifungo cha miaka 20 gerezani ili iwe onyo na fundisho kwa Wanaume wengine wenye tabia kama hiyo ya kuwadhalilisha watoto.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "ALIYEJARIBU KUBAKA MTOTO WA MIAKA 8 AHUKUMIWA JELA MIAKA 20"

Post a Comment