Na, Paulina Mpiwa, Sengerema Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bw. Emanuel Kipole
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza Bwn, Emmanuel Enock Kipole amefuta kamati ndogo zote za utunzaji wa Mazingira na rasilimali za fukwe ziwa Victoria (BMU) Wilayani Sengerema kutokana na kuendelea kushika kasi kwa uvuvi haramu.
Mkuu wa wilaya ametoa maamuzi hayo katika baraza la madiwani lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ambapo
amesema kuwa licha ya kuwepo kamati hizo
lakini bado uvuvi haramu unaendelea
kushamili katika ziwa hilo.
Pia ,Bwn,Kipole ametoa siku tatu kwa diwani wa kata ya chifumfu Robart Madaha kurejesha makokoro yote ya wavuvi haramu yaliyopo katika kata yake na kuyapeleka mwenyewe katika kituo cha polisi cha Wilaya ya Sengerema na kama hatafanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Baada ya kutoa maagizo hayo kwa diwani huyo Mkuu wa wilaya pia ameliagiza jeshi la polisi Wilaya ya Sengerema kuwakamatwa mara moja Afisa mtendaji wa kata na mwenyekiti wa kijiji cha Nyakaliro kwa kile alichodai ni kukumbatia suala la uvuvi haramu katika maeneo yao.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amekemea kitendo cha baadhi ya viongozi wanaosaliti juhudi za kupambana na suala la uvuvi haramu katika ziwa Victoria na kusema kuwa siku zao zinahesabika kwa kuwa usaliti ni chanzo cha kurudisha nyuma mapambano dhidi ya uvuvi huo.
0 Response to "DC SENGEREMA AFUTA BMU ZOTE MAPAMBANO DHIDI YA UVUVI HARAMU."
Post a Comment