NA :SALVATORY KELVIN
Kauli hiyo ameitoa juzi na
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu kwenye Baraza la madiwani la halmashauri
ya Mji wa Kahama baada ya kuunda kamati ya kufuatilia kero mbalimbali
zilizowasilishwa na wananchi mjini humo kuhusia na zoezi la upimaji wa viwanja.
Nkulu amesema kampuni
zinazohusika na upimaji wa viwanja mjini Kahama hazijawahi kulipa kodi ya
serikali tangu zimeanza kutoa huduma hiyo kwa wananchi huku baadhi makampuni
hayo hayana sifa ya kutekeleza zoezi hilo.
Ameongeza kuwa kamati
aliyoiunda Imebaini Makampuni hayo kupata zabuni ya kutekeleza zoezi hilo kwa
kuwasilisha nyaraka batili kwa kushirikiana na baadhi yawatumishi wa idara ya
ardhi ya Halmashauri ya Mji na kuisababishia serikali hasara huku wakijua wazi
ni kosa kisheria.
Baadhi ya Kampuni hizo ni
pamoja na JMZ Survery limited,Conride survery limited,na nyinginezo ambazo
zimepewa zabuni ya kupima viwanja mjini Kahama zote zimezuiliwa kuendelea na zoezi hilo sanajari na kuwasilisha nyaraka
za usajili wao kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji.
Mbali na hilo amemtaka
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba kuwachukulia hatua
kali wakuu wa idara waandamizi waliotajwa na Ripoti yake ambao ni pamoja mkuu
wa idara ya ardhi Joakimu Henjewele na Afisa ardhi mteule Yusuph Luhumba.
Mwisho.
0 Response to "DC KAHAMA ASITISHA ZOEZI LA UPIMAJI VIWANJA LILILOKUWA LINALOENDELEA WILAYANI HUMO BAADA YA KUBAINI KUKWEPA KODI YA USHURU WA HUDUMA"
Post a Comment