Na, Paulina Mpiwa,Sengerema Mwanza.
Mahakama ya
wilaya ya sengerema mkoani Mwanza imemuhukumu mtu mmoja kwenda jela
miaka kumi kwa makosa
mawili likiwemo la
kuandaa sumu kwa
nia ya kufanya
madhara.
Akisoma shitaka
linalomkabili mbele
ya hakamu wa
mahakama ya wilaya hiyo BI MONIKA NDYEKOBORA ,mwendesha
mashitaka wa jeshi
la polisi INSPECTA SILIVESTA
MWAISEJE ,amemtaja mshitakiwa
kuwa ni CHARLES JOHN
mwenye umri wa
miaka 22 mkazi
wa Nyitundu wilayani Sengerema.
INSPECTA MWAISEJE amesema
kuwa mtu huyo anashitakiwa
kwa makosa mawili
kosa la kwanza
ni kula njama
kwa nia ya
kutenda kosa kinyume
na kifungu
namba 382
cha kanuni ya
adhabu kuwa mnamo
februari 9 mwaka
huu majira ya
saa 3:00 asubuhi
huko katika maeneo
ya misheni wilaya
ya sengerema mkoa
wa mwanza walikula
njama na mwenzake
ambaye hajakamatwa kwa
nia ya kumuua
Bw. CHARLES MADEBELE.
Kosa la
pili ni kuandaa
sumu kwa nia
ya kufanya madhara
kinyume na kifungu
namba 227
cha kanuni ya
adhabu kuwa CHARLESI JOHN
kwa makusudi aliandaa
sumu na kuiweka
katika kinywaji aina ya soda
ya pepsi kwa
nia ya kumuua
CHARLES MADEBELE.
Hata hivyo
mshitakiwa amekili kutenda
makosa hayo na
mahakama imemtia hatiani
kwa kutumikia kufungo cha
miaka kumi jela.
0 Response to "JELA MIAKA KUMI KWA KUANDAA SUMU KWA AJILI YA KUUA SENGEREMA. "
Post a Comment