POLISI MWANZA YAUA MAJAMBAZI WAWILI

Na salvatory Ntandu 
MWANZA
Watu wawili waliokuwa wakituhumiwa kwa ujambazi wameuawa wakati wakitaka kujaribu kuwatoroka askari polisi wilayani Ilemela mkoani Mwanza

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza amesema kwamba tukio hilo lilitokea  tarehe 20.01.2016 majira ya saa 2:30  usiku, katika mtaa wa kiloleli “A” kata ya Nyasaka mkoa wa Mwanza na kuwataja majambazi waliouawa kuwa ni Eric Magese miaka 22, na aliyejulikana kwa jina moja la Peter miaka kati 25 hadi 27 wote wakazi wa Mecco jijini Mwanza.

Amesema majambazi hao waliuawa wakati wakijaribu kutoroka askari polisi pindi wakiwapeleka mahali ambapo wenzao wamejificha ili waweze kufanya uvamizi.

Amesema kuwa katika tukio hilo pia ilipatikana silaha moja aina ya short gun yenye namba TZ CAR 103283 ikiwa na risasi tatu ambayo inadaiwa walipora kwenye kampuni ya ulinzi iitwayo Malika Security Service Limited

Msangi amesema majambazi hao walikuwa wakitafutwa na polisi baada ya kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali jijini Mwanza ilikiwemo tukio la Kitangiri mnamo tarehe 19.12.2016 na tukio la tarehe 02.01.2016 katika mtaa wa Nyasaka.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "POLISI MWANZA YAUA MAJAMBAZI WAWILI "

Post a Comment