Na, Paulina Mpiwa,
Sengerema Mwanza.
Mwalimu mmoja
amefikishwa katika mahakama
ya wilaya ya sengerema mkoani
mwanza kwa tuhuma
ya makosa mawili
likiwemo la ubakaj.
Akisoma mashitaka
yanayomkabili mbele ya
hakimu wa mahakama
hiyo BI MONIKA NDYEKOBORA mwendesha
mashitaka wa jeshi
la polisi INSPECTA MARTHA
SLIVESTA amemtaja mshitakiwa
kuwa ni OSKA MKANDYA
alimaalufu kwa jina
la JOHN ambaye
ni mwalimu mwenye
umri wa miaka
24 mkazi wa KASISA wilayani hapa.
INSPECTA MARTHA amesema
kuwa mshitakiwa anashitakiwa kwa
makosa mawili kosa
la kwanza ni
kubaka kinyume na
kifungu 130 na
131 cha kanuni
ya adhabu mnamo
tarehe isiyojulikana kati
ya mwezi wa
9 na 10
mwaka jana majira
ya saa 12:00
jioni katika eneo
la kasisa wilayani
hapa mkoa wa
mwanza alimbaka msichana
ambaye jina lake
limehifadhiwa mwenye umri
wa miaka 17 mwanafunzi wa
sekondari kidato cha
tatu.
Kosa la
pili anashitakiwa kwa
tuhuma ya kumpatia
ujauzito mwanafunzi huyo na kumsababishia kushindwa
kuendelea na masomo
yake.
Hata hivyo
mshitakiwa amekana kutenda
makosa hayo na amerudishwa
rumande kwa kushindwa kutimiza mashariti
ya mahakama hadi
februari 23 mwaka
huu, kesi hiyo
itaendelea kusikilizwa mahakamani hapo.
0 Response to "MWALIMU ATUHUMIWA KUMBAKA MWANAFUNZI WILAYANI SENGEREMA."
Post a Comment