JESHI LA POLISI KAHAMA LANUSURU KUUWAWA KWA MWANAMKE KWA KILE KINACHODAIWA KUWA NI MIGOGORO ARDHI




Na Salvatory  Ntandu :KAHAMA
Jeshi la Polisi wilayani Kahama linawashikilia watu watano akiwemo mwenyekiti wa kitongoji cha Iluguti PASCHAL STEPHANO(40) kwaajili ya mahojiano kuhusiana na tukio la kumtishia kumkata mapanga MINZA SADU (37) kwa kile kinachodaiwa ni migogoro ya ardhi.
Wengine ni Pamoja na MASHAKA PETER (25), BULUGU KASU (40) BIS MAKOYE (25) na TABU MALECHA (40) kwa pamoja wanadaiwa kumpa siku tano MINZA  kuhama kijiji hicho na endapo akikaidi wange muua kwa kumkata mapanaga .
Uamuzi wa kuawakamata watuhumiwa hao Umetolewa Jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kahama, FADHIL NKULU kwenye mkutano wa hadhara na wakazi wa kijiji cha Nyanhembe kilichopo katika Kata ya Kilago.
NKULU amesema serikali itaendelea kuchukua hatua kali watu wanaotekeleza mauaji kwa watu wasiokuwa na hatia kwenye jamii kwa imani za kishirikina jambo ambalo linapunguza nguvu kazi ya taifa sambamba na kuipa sifa wilaya na mkoa kwa ujumla.
Kwa upande wake mkuu wa Polisi Wilaya ya Kahama MUSA MCHENYA ametoa onyo kali kwa waganga wakienyeji wanaopiga ramli chonganishi kuacha kazi hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "JESHI LA POLISI KAHAMA LANUSURU KUUWAWA KWA MWANAMKE KWA KILE KINACHODAIWA KUWA NI MIGOGORO ARDHI"

Post a Comment