Na, Paulina Mpiwa,
Sengerema- Mwanza.
Wakazi wa kitongoji cha
KILABELA kata ya MWABALUHI Wilayani SENGEREMA Mkoani MWANZA
wamemlalamikia mwenyekiti wa
kitongoji hicho kwa kushindwa kuwasomea mapato na matumizi kwa
miezi mitatu.
Malalamiko hayo
yamekuja kufuatia wananchi hao kueleza
kuwa mwenyekiti huyo amekuwa mstari wa mbele kuchangisha pesa pasipokujua mchanganua wa fedha hizo
wanazochanga kwa shughuli mbalimbali.
Wameeleza kuwa kiongozi huyo kushindwa kuwasomea mapato na
matumizi ni kudidimiza maendeleo ya
eneo hilo sambamba na kukaribisha mwanya
wa upotevu wa fedha ambazo zingesaidia katika maendeleo ya kitongoji hicho.
Kufuatia malalamiko
hayo mwenyekiti wa kitongoji hicho Bwn. SAMWEL
MACHENI NZUNGU amekiri kutowasomea mapato na matumizi kwa muda mrefu sasa wananchi wake huku akiahidi
kutekeleza jambo hilo hivi
karibuni .
Aidha sakata la mwenyekiti huyo la kutowasomea taarifa ya mapato na matumizi wakazi wa eneo
lake limeanza kuleta taswira mpya baada ya
baadhi ya wakazi wa eneo hilo
kuahidi kutotoa ushirikiano wa mchango
wowote kuanzia hivi sasa mpaka pale atakapofuata utaratibu.
0 Response to "WANANCHI WAHOJI TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI."
Post a Comment