Na, Paulina Mpiwa,
Sengerema
Wanafunzi wa chuo cha
uuguzi SENGEREMA wilayani SENGEREMA
mkoani MWANZA wameendelea na
mgomo wa kutoingia darasani kushinikiza
kuondolewa kwa walimu wawili wanaosababisha migogoro ya mara kwa mara.
Wakizungumza katika
kikao cha dharura kilichoitishwa na menejimenti ya chuo kwa lengo la utatuzi wa
mgogoro wanachuo hao wamezitaja baadhi ya kero wanazokabiliana nazo kuwa ni
pamoja na vitisho kutoka kwa walimu na kula chakula kisichoendana na gharama waliyolipia.
Imeelezwa kuwa Bw,JOHN CHRISTOPHER amekuwa akitoa kauli zisizofaa
kwa wanachuo hao, na sista LUCRESIA NJAU
anayedaiwa kutokuwa na uwezo wa kufundisha
masomo hasa ya ukunga kitendo kilichopelekea wanafunzi wote kutofaulu
katika mtihani wa kanda.
Kwa upande wake mkuu wa
chuo hicho Bwana SAMWEL MATHEW amekiri uwepo wa changamoto hizo na kuahidi
kuzitatua ili kulinda hadhi ya chuo.
Hata hivyo juhudi ya kuwapata walimu wanaoshutumiwa hazijazaa matunda baada
ya kutokuwa eneo la kikao hicho cha utatuzi wa migogoro.
Kwa upande wake katibu
tawala halmashauri ya wilaya ya
SENGEREMA Bwana ALAN MHINA aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya SENGEREMA katika kikao ameagiza kusimamishwa mara moja
Kwa walalamikiwa ili kupisha utatuzi wa
mgogoro huo.
Chuo cha uuguzi Sengerema kina milikiwa na kanisa katoliki
jimbo la GEITA .
0 Response to "WALIMU WAWILI CHUO CHA UUGUZI SENGEREMA WASABABISHA MGOMO."
Post a Comment