UHAKIKI WA KAYA MASKINI WALETA SIMANZI.

Na Paulina Mpiwa, Sengerema.

Jumla  ya kaya  46   katika  kijiji cha    Bulyaheke  Halmashauri  ya  Buchosa   wilaya  ya  Sengerema  Mkoani  Mwanza zimeondolewa  katika Mpango  wa kunusuru kaya maskini TASAF awamu  ya tatu  kutokana  na   kutokuwa na   vigezo  vinavyotakiwa.


Zoezi   hilo   limefanyika   chini ya usimamizi wa  Uongozi  wa  TASAF   ngazi ya wilaya kwa kushirikiana  na  viongozi wa eneo  husika,  ili  kufanya  uhakiki  wa  kaya  ambazo zilitakiwa kuwemo  na kutokuwemo, agizo  lililotolewa  na  serikali   ngazi  ya  kitaifa.


Baadhi  ya  wananchi    wamelalamika  kuondolewa katika mpango huo kwani wamedai wanavigezo vya kupata fedha hiyo   huku  wengine   wakieleza   wamesahaulika  kuingizwa  ili nao waweze kunufaika kama wengine wanavyoendelea kunufaika.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "UHAKIKI WA KAYA MASKINI WALETA SIMANZI."

Post a Comment