WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUWA WAADILIFU WANAPOANDIKA TAARIFA ZA MAAFA

 
Wandishi wa Habari Wanaoshiriki semina hiyo wakimsikiliza kwa makini mwezeshaji wa senima hiyo
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kufanyakazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kutanguliza maslahi ya taifa hususan wanaporipoti habari za majanga mbalimbali yanayojitokeza.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Kitaifa wa Maafa Harrison Chinyuka kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye warsha ya siku 10 ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali namna yakujua sheria na miongozo wakati wa kuripoti habari za maafa.

Chinyuka amesema waandishi wa habari hawanabudi kuzingatia maadili ya taaluma hiyo pindi wanapotoa taarifa za majanga hususan tetemeko la ardhi,mafuriko na vimbunga ili kuisaidia jamiii inayowazunguka kuepukana na athari zitokanazo na majanga hayo.

Naye Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya habari za jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Rose Haji Mwalimu amesema waandishi wa habari wanapaswa kushirikiana nyakati zote hususan wanapokuwa wanaripoti taarifa mbalimbali zenye maslahi ya taifa kwa umma ili kuzuia kutokea migongano kwenye jamii.

Mwalimu ameongeza kuwa wanahabari wamekuwa wakiripoti habari zinazoleta migongano kwenye jamii pindi linapotokea janga hivyo ni vyema wakashirikiana na viongozi wenye dhamana kama vile kamati za maafa kwa ngazi zote.

Zaidi ya wanahabari 60 kutoka radio 20 za kijamii nchini Tanzania wanapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutambua, kuripoti taarifa sahihi za matukio ya majanga kwa umma kwa ufadhili wa UNESCO kwa kushirikiana na mashirika ya kimaendeleo ya Sweden na Switzerland.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUWA WAADILIFU WANAPOANDIKA TAARIFA ZA MAAFA"

Post a Comment