AJALI ZA BARABARANI ZAPUNGUA MKOANI DODOMA

Washiriki wa semina wakijufunza namna ya kuandika habari muhimu za jamii kabla ya kwenda kuandika taarifa hii
 
Mkoa wa Dodoma umefanikiwa kupunguza ajali za barabarani hadi kufikia asilimia 78 kwa kipindi cha miezi tisa kuanzia mwezi January mwaka 2016.

Mafanikio hayo yameelezwa na Kamanda wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma Harrison Mwakyoma kwa waandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo ya kuwajengea uwezo kuandika masuala muhimu katika Jamii zinazowazunguka hususan maafa, kilimo, afya, elimu na masuala mtambuka, yanayoendelea mjini Dodoma.

Kamanda Mwakyoma amesema kupungua huko kwa ajali za barabarani kumetokana na jitihada za askari wa usalama barabarani kufanyakazi kwa kujituma katika kudhibiti ajali Mkoani Dodoma.

Jitihada hizo ni pamoja na kudhibiti kupakia abiria zaidi ya mmoja maarufu kama mshikaki, waendeshaji bodaboda wa siokuwa na leseni na mwendokasi katika maeneo ya mjini na barabara ziendazo mikoani.

Hata hivyo amesitikishwa na changamoto zinazojitokeza kukwamisha jitihada zilizopo za kudhibiti ajali zaidi barabarani hasa pale baadhi ya abiria wanaposhindwa kutoa taarifa juu ya makosa mbalimbali yanayosababishwa na madereva wakati wengine wakishabikia mwendokasi kwa madereva wanapokuwa katika vyombo vya moto.

Msikilize Kamanda Mwakyoma hapa chini...

Wakitoamaoniyao kwa waandishi wa habari wa Semina Dodoma baadhi ya wakazi wa Dodoma wamelishaurijeshi hilo kutoaelimu ya usalamabarabaraniitakayokuwaendelevu kwa madereva na watumiaji wa barabaraili kudhibitiajaliMkoani Dodoma.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "AJALI ZA BARABARANI ZAPUNGUA MKOANI DODOMA"

Post a Comment