MANISPAA YA DODOMA YAJIPANGA KUKABILIANA NA UTAPIAMLO KWA WATOTO

Wanasemina walioandika taarifa hii wakimsikiliza kwa makini mwezeshaji kabla ya kwenda kufanya mahojiano na wahusika
 Manispaa ya Dodoma imepanga mikakati maalum kukabiliana na tatizo la utapiamlo kwa watoto mkoani Dodoma linaloathiri afya na ukuaji wao.

Hayo yameelezwa na Afisa Lishe wa Manispaa ya Dodoma, Bi Semeni Juma wakati akizungumza na waandishi wa habari wa Semina Dodoma jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo.

Msikilize Semeni Juma Hapa Chini...

Bi Semeni amesema tatizo hilo limechangiwa na upungufu wa chakula unaosababishwa na mvua zisizotosheleza kukuza mazao zinazosababiswa na mabadiliko ya hali ya hewa mkoani humo. hivyo wananchi hawana budi kuhifadhi chakula.

Amewataka wananchi kuhifadhi chakula ili kuhakikisha kuwa makundi maalum kwenye jamii hususan watoto wanapata lishe bora na wanakua vizuri.

Naye Afisa Mazingira Manispaa ya Dodoma Hapiness Karugaba wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kuhusiana na familia nyingi kutengana kutokana na tatizo la uhaba wa chakula.

Msikilize Hapiness Karugaba hapa chini...

Bibi Karugaba ameeleza pia kuwa uhaba wa chakula mkoani Dodoma unasababisha kuwepo kwa wimbi la watoto wanaoishi mitaani ambalo ni janga lingine kwataifa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "MANISPAA YA DODOMA YAJIPANGA KUKABILIANA NA UTAPIAMLO KWA WATOTO"

Post a Comment