WAANDISHI WA HABARI WAHAMASISHWA KUANDIKA TAARIFA ZENYE MASLAHI KWA JAMII

Mkufunzi Bi Rose Mwalimu kutoka UNESCO Akitoa somo katika semina hiyo inayoendelea mjini Dodoma
Waandishi wa habariwa redio za kijamii nchini wametakiwa kuandika habari zitakazo isaidia jamii wanayoihudumia kukabiliana na changamoto zilizoko kwenye maeneo yao.

Kauli hiyo imetolewa na Mtaalam na Mkufunzi wa Masuala ya Habari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO) Bi Rose Mwalimu wakatiwa mafunzo ya siku kumi ya waandishi wa habari kutoka redio 20 za kijamii Tanzania bara na Visiwani jinsi ya kuandika habari zinazogusa maisha ya watu wanaozizunguka redio Jamii mjini Dodoma.

Bi Mwalimu amesema kuwa mwandishi wa habarinimtumuhimu katika jamii hivyo anatakiwa kuandika habari zenye mashiko na kugusa jamii hususan masuala ya afya, kilimo, elimu na masuala mengine mtambuka kama upatikanaji wa maji safi na mengineyo.

Sikiliza Sauti ya Rose Mwalimu hapa...

Ameendelea kusema kuwa waandishi wahabari vijijini wanategemewa na Jamii inayowazunguka kwa kuwa wanaelewa changamoto zilizopo, hivyo ni wajibu wao kuhakikisha kuwa taarifa wanazoziandika na kuzitangaza zinaisaidia Jamii kuelimika na kufanya maamuzi sahihi kwa maendeleo yao.

Semina Dodoma pia imepata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo ambao wamesema kuwa wanategemea kunufaika na elimu watakayoipata na kuitumia kwa lengo la kuleta mabadiliko katika Jamii zao.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "WAANDISHI WA HABARI WAHAMASISHWA KUANDIKA TAARIFA ZENYE MASLAHI KWA JAMII"

Post a Comment