USHIRIKIANO BAINA YA MAMLAKA HUSIKA UNAHITAJIKA KURIPOTI TAARIFA ZA MAAFA

Bi Rose Mwalongo Akitete jambo na Bi Rose Mwalimu Wakati wa mafunzo hayo
Waandishi wahabari na viongozi wenye dhamana hususan kamati za maafa katika ngazizote wanapaswa kushirikiana wakati wote hasa wanaporipoti habari mbalimbali za maafa kwa maslahi ya Jamii na taifa kwa ujumla.

Ushirikiano katika taarifa hizo zitazuia migongano na maslahi miongoni mwa viongozi na Jamii kwa ujumla hasa pale misaada inapohitajika kwa wahanga wa maafa husika.

Hayo yamesemwa katika Warsha inayowajumuisha waandishi 60 kutoka vyombo vya habari vya kijamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar inayofanyika mjini Dodoma, inayolenga kuwa wanapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo kitaaluma namna ya Kuandika taarifa mbalimbali zinazoihusu Jamii inayozizunguka redio za kijamii kwa lengo ya kuboresha taarifa na vipindi vya redio.

Akizungumza wakati wa kufungua Warsha hiyo Mshauri kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Rose Mwalongo amesema miongoni mwa mambo muhimu ya kuzingatia nikuandika taarifa zinazohusu mahitaji muhimu hususan huduma za afya, chakula na makazi ili kunusuru maisha ya waliopatwa na maafa. 

Amesema kutofanya hivyo kunaweza kusababisha watu kupoteza maisha kutokana naucheleweshaji wa kupatiwa mahitaji muhimu na kwa wakati.

Washiriki wametakiwa pia kuwafikia wanajamii na kuwafanyia mahojiano ili kufahamu ni mahitaji gani yana yohitajika badala ya kutegemea taarifa za kupewa kutoka vyanzo visivyo aminika.

Redio za kijamii zinauwezo mkubwa wa kuokoa maisha ya watu kutokana na maafa mbalimbali kwa kutoa tahadhari mapema kwa jamii inayoizunguka hususan pale mvua kubwa inaponyesha, badala ya kusubiri maafa ya mafuriko kutokea.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "USHIRIKIANO BAINA YA MAMLAKA HUSIKA UNAHITAJIKA KURIPOTI TAARIFA ZA MAAFA"

Post a Comment