UHABA WA CHAKULA NI CHANGAMOTO KWA WANAFAMILIA DODOMA

Bi Rose Mwalimu kutoka UNESCO akitoa somo kwa wanahabari walioandika taarifa hii kabla ya kwenda kufanya mahojiano na wahusika
Uhaba wa chakula unaosababishwa na ukame unaendelea Mkoani Dodoma kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ni changamoto kubwa katika ustawi wa familia Mkoani hapa.

Kutokana na kuwepo kwa tatizo la ukame katika mkoa wa dodoma inadaiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa chakula katika mkoa huo hali inayosababisha kusambaratika kwa baadhi ya familia zenye kipato cha chini.

Akizungumza na wandishi wa habari Semina Dodoma, Afisa Mazingira Manispaa ya Dodoma Hapiness Karugaba amesema kuwa hivi karibuni baadhi ya familia zinazishi katika mazingira magumu kutokana na uhaba wa mavuno kidogo inaosababisha na hali ya ukame na kipato kidogo hali inayowafanya baadhi ya familia kushindwa kuhudumia familia zao na kuamua kuzikimbia.
 
Sikiliza sauti ya hapiness Hapa chini...

Wakati huo huo Afisa Lishe wa Manispaa ya Dodoma, Semeni Juma amethibitisha kuwepo kwa mavuno hafifu kutokana na ukame wa ukosefu wa mvua na kusababisha lishe duni na udumavu wa akili kwa wananchi hususan watoto wadogo na anaelezea mikakati ya serikali katika kukabiliana na hali hiyo.

Sikiliza sauti ya Semeini Juma Hapa chini...

Baadhi ya wananchi waishio katika Manispaa ya Dodoma wamesema kuwa hali hiyo inaawaathiri sana kutokana na ukweli kwamba hutegema mvua kwa ajili ya mazao yao.

Sikiliza sauti za wananchi hapa chini...
 
Hali ya ukame Mkoani Dodoma imejitokeza baada ya kuchelewa kunyesha kwa mvua za msimu kunakosababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "UHABA WA CHAKULA NI CHANGAMOTO KWA WANAFAMILIA DODOMA"

Post a Comment