UKAME WASABABISHA UPUNGUFU WA CHAKULA, WATISHIA KUSAMBARATISHA FAMILIA DODOMA

Washiriki kutoka Redio Jamii 20 nchini Tanzania Wakisikiliza Mafunzo mjini Dodoma Kuhusu kuandika Masuala ya Majanga yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya mpango wa SIDA/SDC
Na Waandishi Jamii Dodoma
Tatizo la ukame katika manispaa ya Domoma Mjini, liimechangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa chakula na kuchochea kusamabaratika baadhi ya familia zenye kipato cha chini.

Akizungumza na wandishi wa habari, afisa mazingira manispaa ya Dodoma Bibi Hapiness Karugaba amesema kuwa kutokana na mavuno kidogo yanayosababishwa na hali ya ukame, baadhi ya familia hushindwa kuhudumia familia zao.


Kwa upande wake Afisa Lishe wa Manispaa ya Dodoma,Bibi Semeni Juma amesema uchache wa mavuno unaotokana na ukame unasababisha ukosefu wa lishe bora na udumavu wa akili kwa wananchi hususan watoto wadogo.

Bibi Semeni amesema serikali inajipanga kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na hali hiyo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "UKAME WASABABISHA UPUNGUFU WA CHAKULA, WATISHIA KUSAMBARATISHA FAMILIA DODOMA"

Post a Comment