ELIMU DUNI YA USALAMA BARABARANI, ONGEZEKO LA AJALI DODOMA

Baadhi ya washiriki wa semina inayosimamiwa na UNESCO inayoendelea mkoani Dodoma
Na Waandishi Jamii, Dodoma
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma wameliomba Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya alama  ili kupunguza ongezeko la ajali za barabarani.

Wakizungumza na Semina FM wamesema ajali za barabarani zimekuwa zikiongezeka kutokana na wananchi kutokuwa na elimu sahihi ya matumizi ya alama za barabarani.

Miongoni mwa waendesha pikipiki, Shadrack Hambaya na Severine Joseph wamelilaumu jeshi hilo kwa kuendesha zoezi la ukamataji wa pikipiki kiholela linalochangia waendesha pikipiki kuendesha mwendo kasi na kusababisha ongezeko la ajali za barabarani.

Kwa upande wake kamanda wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma Marrison Mwakyoma amesema wananchi wanapaswa kuzingatia sheria mbalimbali za usalama barabarani kwa lengo la kuokoa maisha ya watumiaji na madereva wa biashara hiyo.
 
Kwa mujibu wa Kamanda Mwakyoma pamoja na kuwepo kwa ajali za barabarani, Mkoa wa Dodoma umefanikiwa kupunguza ajali hizo kwa asilimia 78 katika kipindi kuanzia mwezi Januari hadi Septemba mwaka 2016. 

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "ELIMU DUNI YA USALAMA BARABARANI, ONGEZEKO LA AJALI DODOMA"

Post a Comment