SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI WATENDAJI WAZEMBE WANAORUHUSU WATOTO KUTUMIKISHWA KATIKA KILIMO CHA ZAO LA TUMBAKU




 
TABORA

Na Salvatory Kelvin

Watendaji wa Serikali mkoani Tabora wametakiwa kuhakikisha kuwa wanakomesha tabia ya kuwatumikisha watoto wadogo hususan kwenye kilimo cha zao la tumbaku.
Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, AGREY MWANRI wakati akizungumza kwenye kikao cha wadau wa zao la tumbaku kinachoendelea mkoani humo.

MWANRI amefafanua kuwa wakuu wa wilaya, wabunge na viongozi mbalimbali wa vyama vya ushirika wa tumbaku wanapaswa kupiga vita utumikishwaji huo wa watoto mashambani.

Akizungumza katika kikao hicho, Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, EMANUEL MWAKASAKA pamoja na kuunga mkono kukomesha utumikishwaji wa watoto, amelalamikia msururu wa kodi kwa wakulima wa tumbaku ambazo hazimnufaishi mkulima.

Zao la tumbaku licha ya kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni wakulima wa zao hilo wanakabiliwa na hali duni ya kiuchumi kutokana na wingi wa kodi ambazo hazimnufaishi mkulima.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 Response to "SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI WATENDAJI WAZEMBE WANAORUHUSU WATOTO KUTUMIKISHWA KATIKA KILIMO CHA ZAO LA TUMBAKU"

Post a Comment